Saturday, October 18, 2014

KIPINDI KIPYA CHA BAMBA KWA BAMBA KUJA CHANNEL TEN

Picha ya chini ni Mtangazaji wa Bamba kwa Bamba Khalid Ali akiwa Mtaani
Hiki ndio Kipindi kipya cha Bamba kwa Bamba kinachokuja kwa kupitia Runinga ya Channel Ten mwezi huu. Mtangazaji wa Kipindi cha Bamba kwa Bamba Khalid Ali akiwa kazini. Mtangazaji wa kipindi cha Bamba kwa Bamba akiwa katika ya foleni akirekodi kipindi kwa ajili ya kuruka siku ya Jumamosi. Kampuni ya Saseni Media ya jijini Dar es Salaam imekusudia kuleta amani katika baadhi ya familia ambazo zimekuwa zikijikuta zinaingia katika sintofahamu baada ya mwanafamilia mmoja kuchelewa kurudi nyumbani kwa sababu ya foleni. Kupitia kipindi cha Bamba kwa Bamba ambacho kitaruka kwa nusu saa, jamii itapata kujionea hali halisi ambayo huwakuta abiria warudipo majumbani au asubuhi wanapowahi kwenda makazini, kwani hata kuna siku ambazo unawahi lakini foleni inakukwamisha na kupoteza malengo. Inakadiriwa kwamba wananchi waishio Dar es Salaam hukaa kwenye foleni kwa takribani masaa mawili mpaka matatu kwa siku au zaidi. Swali ni je muda wote huwa wanafanyanini? Au Wafanye nini? BAMPA KWA BAMPA ni kipindi kipya cha Televisheni kinachozalishwa na kampuni ya Saseni Media na kurushwa na Channel 10 siku za Jumamosi saa 12:00 mpaka 12:30 jioni. Bampa kwa Bampa ni kipindi cha kwanza cha Runinga kinachotoa fursa na uwanja wa mawazo kwa Watanzania wote. Ambao kwa muda huo wanakuwa kwenye foleni na walioko majumbani kushiriki katika kujadili na kutoa maoni, mawazo, mapendekezo na ushauri kuhusiana na mada mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa, nakupendekeza nini kifanyike ili kuleta maendeleo ya Taifa la Tanzania, katika Nyanja kadha wa kadha. Msemo wa ‘Bampa Kwa Bampa’ unaashiria namna magari ya kisogelea na kwaukaribu sana kiasi cha bampa la gari mbele (nyuma) na lile la nyuma (mbele) kuacha upenyo mdogo au pikipikikupita. Hii hutokea hasa nyakati za asubuhi na jioni. Mahojiano na watu walioko katika foleni, wakiwa ndani ya vyombo vya usafiribi nafsi au vya abiria, iwe ni gari dogo, kubwa, daladala, bodaboda, bajaj, baiskeli au una kwenda kwa miguu hii inakuwa ni fursa ya kukutana na mtangazaji wa kipindi Khalid Ali. Khalid Ali ni mhitimu wa Digrii ya Mawasiliano kwa Umma ya Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari na mwenye dhamira yakutafiti, kuchanganua, kuibua changamoto na kukusanya maoni na fikra za wananchi kuhusu maendeleo yao akiongozwa na falsafa ya kwamba maendeleo yetu, yataletwa na sisi wenyewe tukizungumza, kukumbushana nakujifunza kwa kupitia TV na hasa kipindi cha Bampa kwa Bampa.Pia wananchi wengine wanaweza kuchangia maoni yao katika mada za kila wiki kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya Bampa Kwa Bampa kwa kutembelea Facebook na Twitter. www.facebook.com/BampaKwaBampa www.twitter.com/bampakwabampa Kipindi hiki kitakuwa kikirushwa kupitia Channel TEN kila siku ya Jumamosi, Saa 12:00 Jioni, kuanzia mwezi Oktoba 2014

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments