Friday, August 3, 2012

MTANGAZAJI PEKEE WA KIUME ANAEKIMBIZA KATIKA VIPINDI VYA TAARAB

P. Lover mtangazaji pekee wa kiume wa vipindi vya Taarab

Ni mara chache kusikia vipindi vinavohusu muziki wa Taarab kutangazwa na watangazaji wa kiume kutokana na imani za wanaume wengi kuamini kuwa Taarab ni muziki wa wanawake.

P. Lover mtangazaji wa HITS FM ni mmoja wa watangazaji wa kiume anaewashangaza watu wengi baada ya kuonyesha ubunifu mkubwa wa utangazaji wa kipindi cha Taarab na kuwa na upinzani mkubwa na vipindi kama hivyo vilivyozoeleka kusikika sauti za wanawake, hii ni moja ya ujasiri wa kuonyesha kwamba watu wasiishi maisha ya kukariri kwani kila kitu kinawezekana kwa kila mtu ili mradi kisiwe ni dhambi.

Endapo ingalikuwa muziki wa Taarab ni muziki wa wanawake basi hali hiyo ingalipelekea wanaume wasingaliimba muziki wa aina hiyo, lakini kutokana na kwamba muziki ni kipaji na kipaji hakichagui jinsi kinaweza kuwa kwa mwanaume ama mwanamke na  ndio maana wapo wasanii wengi wa kiume wanaoimba muziki wa aina hiyo.

Mfalme Mzee Yusuf ambae ni mmiliki wa JAHAZI MORDEN TAARAB ni miongoni mwa waimbaji wa kiume wa muziki huo, nani asiye mfahamu Mfalme Mzee Yusuf katika tasnia ya muziki wa Taarab nchini Tanzania na hana mpinzani kutokana na umahiri wake katika utunzi wa mashari mazuri yanayowavutia wanawake na wanaume WHY hajawahi kusita kuimba muziki huo.

Wapo waimbaji wengi wa kike wa muziki wa Taarab kama Malkia Khadija Kopa, Isha Mashauzi na wengine wengi wanaofanya vizuri katika muziki huo. Hali ya upinzani kwa wasanii hawa wakike na Mfalme Mzee Yusuf na waimbaji wengineo wa kiume inafahamika katika jamii ya Tanzania.

Hali hii inadhihirisha kuwa hata kwa upande wa utangazaji pia ni kipaji ambacho anakuwa nacho mtu bila ya kulazimisha wapo wenye uwezo mkubwa wa kutangaza vipindi vinavyohusu muziki wa Hip hop, R & B, Dansi na aina nyinginezo ambao ni wengi kila kona tofauti na upande wa muziki wa Taarab ambako wanaume wengi wanajenga hofu ya kuonyesha vipaji vyao kwa kutangaza vipindi vya muziki huo.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments