Monday, August 8, 2016

Mwanamuziki Lil Bow Wow kustaafu muziki akiwa na miaka 29

Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za 'hip hop' Bow Wow, ambaye jina lake halisi ni Shad Moss, ametangaza kuwa atastaafu kutoka kwenye fani ya muziki akiwa na umri wa miaka 29, mwaka huu 2016.
Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.
Bow Wow alitoa albamu yake ya kwanza 'Beware of Dog' septemba 29 akiwa na umri wa miaka 13, mwaka 2000.
Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni "Like You" akimshirikisha Ciara na "Let me hold you" akimshirikisha Omarion Bow wow "That's my name" akimshirikisha Snoop Dogg.
Bow wow amedumu kwa muda wa miaka 23 katika game na kuachia albam zaidi ya 5.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments