Tuesday, July 5, 2016

Msanii wa bongo muvi King Desamo aachia hit song "Ugali Kunguru"


Msanii maarufu wa bongo muvi King Desamo aachia wimbo wake "Ugali kunguru" aliomshirikisha Nyota.

Wimbo huo umetengenezwa na producer Hassa B katika studio za Tone records akiwa anaelekea kukamilisha albamu ya kwanza itayobeba jumla ya nyimbo 25 itakayotoka mwishoni mwa mwezi huu.

Desamo alianza kujihusisha na muziki mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 15 kabla ya kuwa muigizaji, mwaka 1999 kwa mara ya kwanza alikutana na producer Kameta kinondoni jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kurekodi wimbo "mambo bayana", mwaka 2000 alirekodi ngoma nyingine Fm Studio chini ya producer Double B wimbo aliouita Utajidai Vipi? 

Kwa sasa ni muigizaji mahiri mwenye filamu zaidi 6 ikiwemo Emorata, Hasidi, Back to Life, Enternal Love, Ampicilin, Bado Natafuta, Tajiri Mfupi, Siku Itafika, Elisheva na nyingine.
Kava ya Back to life

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments