Thursday, September 5, 2013

Taarifa toka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro


Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA) ina utaratibu wa kushirikiana
na jamii zinazozunguka hifadhi, ikiwa ni
pamoja na asasi za kiraia, taasisi za
serikali, mahospitali, mashule, na vijiji
kote nchini kwa kuchangia katika
shughuli zao za maendeleo. Michango
inayotolewa na Mamlaka inalenga
kuwawezesha wananchi kupitia vijiji,
asasi, ama taasisi husika kwa kusaidia
miradi mahususi iliyoainishwa kupitia
maombi yao kwa Mamlaka na
kupitishwa ofisi ya Mhifadhi Mkuu.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
inatoa misaada hiyo kama sehemu ya
majukumu yake ya kushirikiana na
wanajamii (corporate social
responsibility). Aidha, Mamlaka
imeendelea kutoa misaada hii kwa
kutegemea uwezo wa kifedha, mkazo
mkubwa ukiwa kwenye miradi ya Jamii
zinazozunguka hifadhi, na vilevile,
kusaidia miradi, majanga, na shughuli
zingine kote nchini. Kulingana na
maombi na uwezo wa fedha wa
Mamlaka.
Hivi karibuni kumetokea taarifa potofu
kwenye vyombo vya habari na mitandao
ya kjamii kwamba Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro inatoa msaada hiyo kwa
baadhi ya Taasisi kwa mashinikizo ya
kisiasa, taarifa ambazo hazina ukweli
wowote na zina lengo la kufarakanisha
Mamlaka na Wananchi ambao
wamekuwa wakipokea misaada ya
kibinadamu na kimaendeleo kwa kupitia
utaratibu wa ujirani mwema wa
Mamlaka.
Habari hizi zinasikitisha, na si sahihi.
Tunapenda kutoa rai kwa umma
kwamba Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro itaendelea na jukumu lake
la kusaidia jamii mbalimbali nchini,
ikiwa ni pamoja na kuendelea kushiriki
katika shughuli za maendeleo, na
kuwanusuru wananchi pale ambapo
majanga yanatokea kama ilivyokuwa
katika milipuko ya mabomu iliyotokea
katika Jiji la Arusha hivi karibuni.
KAULI MBIU YETU
“UTALII UANZE NA MTANZANIA
KWANZA”
Imetolewa na Kaimu Mhifadhi
MAMLAKA YA HIFADHI YA
NGORONGORO

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments