Saturday, August 31, 2013
Mrithi wa "Mr Ebbo" Kajoli Masai Ft Queen A-Kama Unanipenda
Unapomsikiliza "Kajoli Masai" Msanii anayewakilisha Arusha kwa kuimba style ya ladha ya lafudhi ya kimaasai, Kwa haraka utamkumbuka marehem Mr Ebbo ambae aliwakilisha vema kabila la masai katika anga ya mziki wa bongo.
Msanii Kajoli kutoka kabila la masai ameamua kuchukua fursa ya kuendeleza ladha ya masai katika muziki wa Tanzania hapa ameshirikiana na mwanadada Queen A katika wimbo wake "Kama Unanipenda" download HAPA kwa mawasiliano check na Kajoli kupitia + 255 755 497 334 endelea kusapoti muziki wa Tanzania. www.vmgafrica.com
Friday, August 30, 2013
Benpol-Twaendana (KIONJO-SNIPPET)
Sikiliza Kionjo cha wimbo utakao achiwa hivi karibuni na mkali BenPol, ngoma hiyo ameipa jina la "Twaendana",kazi toka Noizmekah Production Studios Arusha, Chini ya Producer DefXtro, download HAPA, www.vmgafrica.com (KIONJO) Benpol-Twaendana
Basi la Simba Mtoto lazima katikati ya daraja maeneo ya Kibamba na kusababisha foleni kubwa
Basi la abiria la kampuni ya Simba mtoto litokalio Dar es salaam kuelekea Tanga likiwa limepata hitilafu na kuzimika katikati ya daraja maeneo ya Kibamba na kusababisha msongamano mkubwa wa magari jana jioni.
Hali hiyo ilidumu kwa muda wa zaidi ya dk 20 mpaka basi hilo lilipowaka na kusogezwa pembeni.
Monday, August 26, 2013
FidoVato-Biz Za Machiz (Official Video & Audio Link)
FidoVato toka Vatoloco the red anadrop full package ya "Biz Za Machiz" ikiwa ni Audio & Video project ilorekodiwa Noizmekah Studio na video pia kufanywa Noizmekah-Hoodpixx VMG chini ya Defxtro, Pata kudownload ngoma HAPA Video link Hii ni Hardcore Hiphop Material for all the real Hiphop Fans in the world, Kwa mawasiliano/Mahojiano zaidi check na FidoVato kupitia www.vmgafrica.com
Biz Za Machiz AUDIO-
Biz Za Machiz VIDEO-
Sunday, August 25, 2013
Cheki mapokezi ya Diamond yalivyopokelewa mjini mpanda
Hakika kwa lililotokea mkoani mpanda basi si
la kusahau kila rahisi,kwa historia kufutika
kichwani mwangu
na milele moyoni Mwangu.
Siku ya Jana wakati nimetokea jijini Tabora
kwenye Fiesta 2013
baada ya kibarua ,hapa tena nakuja
Mpanda nikiwa na crew yangu nzima.
Majira ya saa 7 tulikuwa tumewasili uwanja
wa ndege
wa Binafsi Mkoani humu lakini baada
ya Kuwasili na kutokeza tu nje,ghafla hali
ya hewa
ilibadilika kuwa ya Furaha na watu
kujazana
kwenye uzio wa uwanja wa ndege mdogo endelea hapa
Saturday, August 24, 2013
Mazishi ya Nasra Hamis Rajabu yalivyokuwa
Umati wa watu walijitokeza jana katika maziko ya mjomba wa Dj Dk B yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kwaminchi mjini Tanga.
Nasra Hamis alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua pamoja na malaria alilazazwa hospitali ya bombo kwa muda wa wiki moja hadi umauti ulipo mfika.
Mungu amlaze mahala pema peponi amina.
Friday, August 23, 2013
Semina ya fursa ilivyokuwa mkoani Tabora
Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini
Mrisho Mpoto akizungumza kwa
msisitizo,masuala ya fursa mbalimbali
zinazopatikana katika suala zima la
ujasiliamali mapema leo kwenye semina
ya Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa
Student's Center,uliopo katikati ya mji
wa mkoa wa Tabora mapema leo.Semina
hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media
Group,imefadhiriwa na shirika la
NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.bofya michuzi http://issamichuzi.[blogspot.com/2013/08/semina-ya-fursa-kwa-vijana.html?m=1]
Thursday, August 22, 2013
Burudani ndani ya Isumba Lounge kama kawaida
Tukutane isumba lounge zamani jollies club every friday and saturday and lets do it (just like back in da days
Wednesday, August 21, 2013
Full moon party on Suturday 24 Kendwa Rock Hotel North of Zanzibar
My life is proof that you can party as a profession. welcome to full moon party on Saturday 24.. Kendwa rock hotel North of Zanzibar.. Entrance 10000 per 1 pax...Massive crowds, Energy music , Acrobatic shows.. Break dancers Dj side and Dj Ally Night long..... Great atmosphere...BBQ PIZZA .ALL KIND OF DRINKS ...I will see U at the bar!
"Excellent" Banx ft Defxtro
Tarehe Moja Mwezi wa Tisa 2013, Banx atadrop "Excellent" ikiwa ni mkono toka Noizmekah Studios akishirikiana na Defxtro alopita Verse moko, Pata Kionjo/Snippet HAPA,kwa mawasiliano/Mahojiano check na www.vmgafrica.com
Tuesday, August 20, 2013
Taarifa ya ajali katika msafara wa mbio za mwenge wa uhuru mkoani Dodoma
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa
Dodoma Bi. Suzzan Kaganda Akiongea
na waandishi wa Habari hawapo
pichani, Katika ukumbi wa Mikutano wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Kuhusia
na ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu,
Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino,
ambapo takribani magari matano (5)
yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge
wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma
kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya
ya Mpwapwa, ambapo Watu wapatao
tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo...endelea hapa
Basi la Turu lachomwa moto na wanakijiji kulipizia kuuwawa kwa mwenzao
Abiria wapatao 60 waliokuwa
wanasafiri na basi la Turu linalofanya
safari zake kati ya mkoa wa Singida na
Haydom mkoani Manyara,
walilazimishwa kuteremka toka ndani
ya basi hilo na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 ) wa vijiji vitatu tofauti ambao
baadae walilichoma moto basi hilo.
Taarifa toka eneo la tukio zinasema
wananchi hao wa vijiji vya Singa,
Idabagadu na Nkungi mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria
wote wameshuka, walilichoma moto basi
hilo ambalo limetekea sehemu kubwa.
Sababu ya wananchi hao kuchukua
uamuzi huo ni kutokana na basi hilo
kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita.
Chanzo michuzi blog
Baada ya kimya kirefu Banx anakuja na mzigo mpya "Area Code"
Banx na Area Code Juu ya Riddim raggaton beat aka Hookmaster toka pande za Arachuga akiwakilisha vilivyo +255, "Nipo likizo fupi kabla ya kuanza ajira rasmi hivo nimefeel ni muda tangu kurecord,fans wamemiss ladha kibao so hi ngoma club banger iko ready to set floors on fayaaaa,holla na banx" download Area Code HAPA, www.vmgafrica.com endelea kutoa sapoti muziki wa Tanzania.
Monday, August 19, 2013
Wavuvi Ujerumani wavua Samaki mwenye mkubwa mwenye uzito wa kg 233.5 wavunja record ya dunia
Wavuvi wa nchini Ujerumani wamevunja rekodi baada ya kumvua samaki mkubwa na kuweka rekodi ya dunia katika
samaki wakubwa walio wahi kuvuliwa.
Samaki huyo mwenye uzito wa kilo 233.5 na urefu wa mita 2.63 ameiweka Ujerumani katika rekodi hiyo ya dunia wakati Samaki wengine waliowahi kuvuliwa na kuweka rekodi dunia walikuwa na uzito wa kilo 108, kilo 190, kilo 211 na wengineo .
Wavuvi hao wanasema ilichukua zaidi ya saa 1 katika harakati za kumvua samaki huyo. Kiongozi
wao anasema walidhani ndoano yao imenasa kwenye manowari kutokana na ugumu na uzito uliokuwepo wakati wa kuivuta
Sunday, August 18, 2013
JCB & Moplus ft Catrina-Mapinduzi
Ngoma Mpya Toka kwa JCB & Moplus from the "Makalla wa Ukoo Mixtape, ikiwa ni collabo na mwanadada Catrina, kazi inaitwa "Mapinduzi" na imerekodiwa juu ya beat ya Zigilaa katika studio za Noizmekah kwa Defxtro, sikiliza ngoma HAPA www.vmgafrica.com
Saturday, August 17, 2013
KCK na "Mitaa Inauliza" KIONJO.SNIPPET
KcK, kundi kongwe la HipHop Music Arusha linaloundwa na Spacdawg pamoja na Boox wanadrop ngoma "Mitaa Inauliza" toka Noizmekah Productions hivi karibuni kwa maana album pia ni legendary album yenye format ya tofauti kabisa, nyenzo mpya mbalimbali za kiteknolojia zimezingatiwa na sasa tupo katika mastering kukamilisha mpango mzima wa mawe 31, sikiliza kionjo cha Mitaa Inauliza HAPA kwa mawasiliano/mahojiano zaidi piga simu +255 754 970 956 au +255 756 022 224 www.vmgafrica.com
Msaragambo unalegalega baadhi ya maeneo
Mh Saidi Kalembo alipokuwa mkuu wa mkoa wa Tanga aliwatengenezea wakazi wa mkoa huo utaratibu wa kusafisha mazingira kwa eneo lote linalomzunguuka kila mkazi na kushirikiana katika maeneo yasio na mkazi.
Utaratibu huo ulikuwa ukifanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi na ikapewa jina la KALEMBO DAY.
Hali hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kuweka jiji katika hali safi na yakupendeza.
Baada ya kaondoka Mh Kalembo na kuingia Mkuu wa mkoa mwingine ambae ndio anasimamia mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa nae hakuwa nyuma kuisapoti siku hiyo ya usafi iliyoitwa 'Kalembo day'
Kwa lengo la kuzidi kuimarisha hali ya usafi Mhe. Chiku Gallawa aliona ni vema kujenga utaratibu huo kuwa kila jumamosi iwe ni siku ya usafi wa mji na kuita jina 'MSARAGAMBO'.
Hivyo shughuli zote zitaanza saa 3 asubuhi baada ya shughuli ya usafi kumalizika ikiwa ni amri iliyotolewa na Mh mkuu wa mkoa.
Pamoja na jitihada zote hizo hali ya msaragambo inaonekana kulegalega hali inayopelekea baadhi ya maeneo kuendelea kuwa machafu
Pichani ni moja ya eneo la shule ya msingi Chumbageni linaonekana kusahaulika na kuendelea kuwa na hali ya uchafu.
Friday, August 16, 2013
Jaa kubwa katika ya mtaa maeneo ya chumbageni Tanga.
Tanga ni Jiji linalosifika kwa kuwa na mazingira safi yanayopendeza kila kona ya mtaa lakini eneo hili lililopo mtaa wa chumbageni ambalo limezunguukwa na makazi ya watu limekuwa maarufu kwa kutupwa takataka ovyo hali inayopelekea kuwa ndio dampo la mtaa.
Pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na city kuziondoa taka hizo kila zinapokuwa zimezidi inaonekana kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo kwa magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na uchovu wa mazingira hususana kwa watoto wadogo ambao mara kwa mara wanaonekana kupita katika taka hizo na kuokoteza vitu mbalimbali vya kichezea.
Wabunge 11 wa Tanzania wanusurika baada ya bus waliokuwa wakisafiria kutaka kuungua moto
Wakati msafara wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Miundombinu ukielekea Wilayani
Missenyi kukagua sehemu utakapojengwa
uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa
Omukajunguti, gari aina ya Costa lenye
namba za usajili T 570 BYU lilowabeba
Waheshimiwa Wabunge 11 lilipata hitilafu
na kutaka kuungua.
P. T
Ajali hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu
kilometa moja kutoka mpakani mwa
Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi
ambapo gari hilo aina ya costa lilianza
kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma
wakati likiwa kwenye mwendo mkali na
kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo
ndani ya gari hilo .
Mara baada ya dereva kugundua kuwa gari
analoendesha linataka kuungua
alilisimamisha na kuwaambia abiria wake
kuwa gari linaungua.endelea hapa G5 click
Big Daddy Don "Ma Life"
Rapper kutoka kundi la WestPasu anajulikana kama BigDaddy Don aka Malai Junior anaewakilisha vema mkoa wa Moshi ameachia brand new hit inayoitwa "Ma Life"
Ngoma amerekodia Arusha, katika studio za Noizmekah chini ya Producer Defxtro,
Ngoma hii ni Hiphop yenye kionjo kidogo cha kuimba kutoka kwa mchizi mkali wa kusimamia chorus, Chozi.
Pata kuwa wa kwanza kudownload na kusikiliza HAPA
Kwa mawasiliano na mahojiano zaidi na Big Daddy Don check naye kwa Simu nambari +255 763 302 950 www.vmgafrica.com
Thursday, August 15, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)