Saturday, August 17, 2013

Msaragambo unalegalega baadhi ya maeneo




Mh Saidi Kalembo alipokuwa mkuu wa mkoa wa Tanga aliwatengenezea wakazi wa mkoa huo utaratibu wa kusafisha mazingira kwa eneo lote linalomzunguuka kila mkazi na kushirikiana katika maeneo yasio na mkazi.

Utaratibu huo ulikuwa ukifanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi na ikapewa jina la KALEMBO DAY.

Hali hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kuweka jiji katika hali safi na yakupendeza.

Baada ya kaondoka Mh Kalembo na kuingia Mkuu wa mkoa mwingine ambae ndio anasimamia mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa nae hakuwa nyuma kuisapoti siku hiyo ya usafi iliyoitwa 'Kalembo day'

Kwa lengo la kuzidi kuimarisha hali ya usafi Mhe. Chiku Gallawa aliona ni vema kujenga utaratibu huo kuwa kila jumamosi iwe ni siku ya usafi wa mji na kuita jina 'MSARAGAMBO'.

Hivyo shughuli zote zitaanza saa 3 asubuhi baada ya shughuli ya usafi kumalizika ikiwa ni amri iliyotolewa na Mh mkuu wa mkoa.

Pamoja na jitihada zote hizo hali ya msaragambo inaonekana kulegalega hali inayopelekea baadhi ya maeneo kuendelea kuwa machafu

Pichani ni moja ya eneo la shule ya msingi Chumbageni linaonekana kusahaulika na kuendelea kuwa na hali ya uchafu.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments