Saturday, August 10, 2013

Jose Chameleon kupagawisha Dar Escape One leo Eid Pili

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda, Dr. Jose Chameleon anatarajiwa kufanya
onyesho kali kesho kwenye ukumbi mpya
wa burudani wa Escape Complex.
Chameleon, ambaye ndie mwanamuziki
mashuhuri kuliko wote kwenye ukanda
huu wa Afrrika Mashariki anatarajiwa
kukonga nyoyo za wakazi wa Dar es
Salaam kwa kuimba nyimbo zake zote
kali, ikiwemo Valuvalu.
Usiku huo wa Chameleon utaenda
sambamba na burudani kali kutoka kwa
MA DJ wakali, DJ Pac na DJ Senorita
ambao watafanya show ya utangulizi.
Akizungumzia burudani hizo, Meneja
Uendelezi wa Biashara wa Escape
Complex, Anthony David, alisema watu
watarajie burudani kali siku ya
jumamosi hasa kwa kuwa sherehe hizo
zitaenda sambamba na sherehe za Eid
za pale Escape Complex.
‘Kama lilivyo jina lake, Escape ni mahali
ambapo mtu anakuja kupumzika
kukwepa mihangaiko ya kila siku, iwe
kikazi au kimaisha, lakini Eid hii
tumeandaa burudani hii ili kuwapa
wakazi wa Dar es Salaam kitu tofauti’
anasema Anthony.
Mbali na Chameleon siku ya jumamosi,
Escape Complex imeandaa burudani siku
ya Eid Mosi, ambapo DJ maarufu Boni
Luv atatoa burudani kali, na siku ya
Jumpili, bendi inayokuja kwa kasi
Skylight, itawaburudisha wapenzi wake
kuanzia asubuhi ili kuimaliza wikiendi
ndefu.
Escape Complex, ambayo ipo Mikocheni/
Kawe karibu nyuma ya ukumbi wa
Safari Carnival, ni Club mpya ambayo
inapendezeshwa na ufukwe pamoja na
mandhari ya kuvutia, pamoja na
chakula kizuri kwa wateja wake.
Mashabiki wa Chameleon watalipia
shilingi elfu kumi na tano ili
kuburudishwa na mwanamuziki huyo
mashuhuri. Na VIP watalipa elfu 40,000/
= ikiwemo kinywaji cha bure pamoja na
nafasi ya kumuona msanii huyo baada
ya maonyesho.
Source MUHIDIN MICHUZI

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments