Kocha wa Manchester United David Moyes
hii leo ameanza rasmi kibarua chake kama
kocha wa timu hiyo kwenye mechi ya
ushindani baada ya kuiongoza timu hiyo
kupata ushindi wa wa mabao mawili kwa
bila katika mchezo wa kuwania ngao yay
jamii dhidi ya Wigan Athletic .
United ilifunga mabao yake kupitia kwa
mfungaji bora wa ligi kuu ya England kwa
msimu uliopita Robon Van Persie ambaye
alifunga mabao yote mawili .
United iliingia kwenye mchezo huo bila
mshambuliaji wake Wayne Rooney ambaye
hakuchaguliwa kwa kuwa ni majeruhi
huku mustakabali wake ndani ya klabu
hiyo ukibakia kuwa kitendawili
Endelea hapa
No comments:
Post a Comment
Toa maoni yako/ Leave your comments