Friday, August 9, 2013

Kajala na mwanaye wachanganya watu


Na Hamida Hassan
Staa wa filamu za Kibongo , Kajala
Masanja na mwanaye Paula Paul wamekuwa kama mtu na mdogo wake kutokana na kulingana
vimo na kufuatana kila kona kiasi cha kuzua maswali kwa watu

Kajala na mwanaye Paula Paul.

Hivi karibuni wawili hao waliambatana
kwenye mwaliko wa futari iliyoandaliwa na msanii wa filamu, Aunt Ezekiel na kuwafanya mastaa wengine kudhani ni mtu na mdogo wake .
“Ni vigumu kuamini kama huyu ni
mwanao, miye nilipomuana nilidhani
umekuja na mdogo wako , kweli kuzaa
mapema ni mali ,” alisema msanii Devota
Mbaga kwa niaba ya wengine waliokuwa wakishangaa.

Paula Paul
“Huyu ni mwanangu jamani nani hajawahi kumsikia? Wengi wanadhani ni mdogo wangu, najivunia kuwa na binti mkubwa kama huyu kwani naweza kuongea naye kama rafiki yangu ,” alisema Kajala
Source G5 click

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments