Friday, August 16, 2013

Wabunge 11 wa Tanzania wanusurika baada ya bus waliokuwa wakisafiria kutaka kuungua moto


Wakati msafara wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Miundombinu ukielekea Wilayani
Missenyi kukagua sehemu utakapojengwa
uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa
Omukajunguti, gari aina ya Costa lenye
namba za usajili T 570 BYU lilowabeba
Waheshimiwa Wabunge 11 lilipata hitilafu
na kutaka kuungua.
P. T

Ajali hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu
kilometa moja kutoka mpakani mwa
Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi
ambapo gari hilo aina ya costa lilianza
kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma
wakati likiwa kwenye mwendo mkali na
kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo
ndani ya gari hilo .
Mara baada ya dereva kugundua kuwa gari
analoendesha linataka kuungua
alilisimamisha na kuwaambia abiria wake
kuwa gari linaungua.endelea hapa G5 click

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments