Wednesday, July 4, 2012

KIKOSI 'B' CHA YANGA CHATOLEWA JASHO NA JAMHURI KATIKA KOMBE LA TAIFA!

Ubao wa kusomea matokeo 'Score Board' katika uwanja wa Amaan, ukisomeka Jamhuri 
2-1 Yanga, hapa ilikuwa ni dakika 10 ya kipindi cha pili, mpaka mwisho wa mchezo huo Jamhuri 3-2 Ynga.

Kikosi cha pili cha mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati, Dar Young Africans kinachojiandaa na michuano ya Rollingstone kimekubali kufungwa goli 3-2 na Jamhuri ya Pemba, katika mchezo wa kombe la urafiki uliokwisha hivi punde.

Katika mchezo huo Yanga walikuwa wa mwanza kupata goli katika dakika ya 18 mfungaji akiwa Shaban Hamisi.

Jamhuri walifanikiwa kusawazisha goli hilo katika dakika ya 34, na kuongeza jingine katika dakika ya 45. Hivyo kupelekea Yanga kwenda mapumzika wakiwa nyuma kwa goli 2-1.

Katika dakika ya 69 Jamhuri walifanikiwa kuandika goli la tatu huku Yanga wakifunga goli lao la pili katika dakika ya 77 kupitia kwa Notekelly Masasi, na kupelekea mpira kumalizika kwa Yanga kufungwa goli 3-2.

Mwandishi
Ali Mohamed (Mkurugenzi wa fitna)

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments