Monday, July 2, 2012

PRODUCER WA T-TOP REC CHIEF ELIA AFUNGIA FUNGUO YA STUDIO NDANI

Producer wa T-TOP Rec Chief Elia akihangaika kutafuta namna ya kufungua kitasa cha mlango wa kuingilia studio baada ya kufungia funguo ya mlango huo kwa ndani, kazi hiyo ilipelekea baadhi ya wasanii walikuwa wamekwenda hapo kukaa nje kwa zaidi ya dakika 15 huku wengine wakishirikiana nae kutafuta namna ya kufungua kisu ndio zana pekee aliyokuwa akitumia kwa kujaribu kupenyeza ili apate nafasi ya kuweza kutoa loki ya kitasa.
Baada ya muda kadhaa Chief Elia alifanikisha zoezi hilo lililomtoa jasho kiaina na kuingia studio hapo na kuwasha mitambo tayari kwa ajili ya kuwasikilizisha wasanii walikuwapo hapo baadhi ya kazi mpya alizofanya: Rico single, Ismail, Cool Kaka aka Mafian Rapa na Dj Dr B.
Producer huyo akifungua software aina ya studio one anayotumia kufanyia mixing
Chief Elia alikuwa makini baada ya kuplay ngoma Muba Criss aliyomshirikisha Rico Single kwa ajili ya kumsikilizisha Rico Sinlge mwenyewe pamoja na wasanii wengine walikuwepo hapo. Katikati ya nyimbo utamu umekolea mara umeme huo umesepa watuu  ayaaaaaaaaaaa.

1 comment:

Toa maoni yako/ Leave your comments