Sunday, July 28, 2013

Mtuhumiwa wa wizi anusurika kufa kwa kipigo cha wananchi


Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa watu wenye hasira.
MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-
Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam.
Mtu huyo ambaye jina lake halikueza kupatikana mara moja inadaiwa
alikutwa akiruka geti kuingia ndani
kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya
matukio wakati mtuhumiwa huyo
alipokuwa akipata kichapo hicho.

Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi hao wenye hasira.

Mtuhumiwa wa wizi akiomba
kusamehewa wakati mtu mwenye hasira akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo

Lakini kutokana na kipigo akaanguka
hadi hatua iliyofanya watu hao wenye
hasira kutawanyika eneo la tukio,
wakidhani mtuhumiwa amekufa. PICHA
ZOTE NA BASHIR NKOROMO.
Chanzo michuzi blog.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments