Monday, July 1, 2013

Treni ya Mwakyembe yapata ajali

Leo mnamo saa 11:30 asubuhi vichwa
viwili vya treni ya huduma la jiji la Dar
es Salaam vilipata ajali ya kugongwa na
roli la mizigo aina ya Fusso katika
makutano ya reli na barabara ya
Kawawa jijini Dar es salaam , katika jali
hiyo dereva wa Fusso alifariki duniani
papohapo hata hivyo Utingo wake
alinusurika.
Hata hivyo vichwa hivyo vya treni
vilipata mkosi tena wa ajali ambapo
viligongwa na basi dogo la Daladala aina
ya Isuzu katika makutano ya reli eneo la
Kamata. Tukio hilo lilisababisha
majeruhi kadhaa katika basi hilo la
daladala ambapo majeruhi  wamelazwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbil
wakiwemo askari wawili Polisi kutoka
Kikosi cha Reli mmojawapo akiwa
mahututi.
Vichwa hivyo viifanikiwa kufika
stehesheni kwa wakati na kuanza kutoa
huduma ya usafiri wa treni jijini kutoka
Dar Stesheni kwenda Ubungo Maziwa
hadi saa 5 asubuhi hata hivyo huduma ya
leo jioni Julai 01, 2013, imesogezwa
mbele na itaanza saa 12 jioni badala ya
saa 10:30 alasiri.
mabadiliko haya yamebidi yafanyike
kufuatia Jiji la Dar es Salaam kuwa na
hekaheka ya kumpokea Raisi wa
Marekani Barack Obama.
Aidha uongozi wa TRL unawataarifu
wakazi wa jiji kuwa kesho Julai 02, 2013,
huduma za treni ya jiji hazitakuwepo
hadi keshokutwa Julai 03, 2013, ambapo
zitaendelea kama kawaida.
Imtolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba
ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.
Makao Makuu ya TRL
Dar es Salaam.
Julai 01, 2013.

Published with Blogger-droid v2.0.10

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments