Monday, July 29, 2013

Naibu mkuu wa Mji akagua mradi wa maji walaya ya Rombo


Naibu waziri wa maji Dk Binilith
Mahenge akikagua miradi ya maji katika wilaya ya Rombo.

Mhandisi wa maji wilaya ya Rombo
Andrew Tesha akitoa maelezo kwa
naibu waziri wa maji Dk Binilith
Mahenge alipotembelea miradi ya maji katika wilaya hiyo.

Naibu waziri wa maji Dk Mahenge akikagua mradi wa maji
wa kilichopo eneo la hifadhi ya mlima Kilimanjaro(KINAPA).

Habari na Picha Na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii Moshi.


WIZARA ya maji,imeelezea
kutoridhishwa kwake na uendeshaji wa
kampuni ya usambazaji maji wilayani
Rombo ya Kiliwater kwamba
haijajipanga kibiashara na ingeweza
kupata faida kubwa kuliko hali
waliyonayo sasa kama wangekuwa
makini.
Naibu waziri wa maji Dk Binillith
Mahenge alitoa kauli hiyo baada ya
kupokea taarifa ya kampuni hiyo kuhusu
usambazaji wa huduma za maji na
mipango yao katika ununuzi wa mita
kwa ajili ya kuwafungia wateja wao.
“Kwa mipango hii mliyonayo kama
kampuni hii ingekuwa imekabidhiwa
mfanyabiashara yeyote
makini,angeshindwa kupata faida?”
alihoji huku mwenyekiti wa bodi ya
kampuni hiyo, Silayo akikiri kwamba
faida ingepatikana.
Aliitaka kampuni hiyo kujipanga upya
kwani wanayo fursa ya kupata faida
kama wakijitahidi kupunguza maji
yanayopotea lakini pia kuhakikisha
wanaondokana na mfumo wa ulipaji
anka kwa ‘Flat rate’ bali wawafungie
wateja mita za maji.
“Huu mfumo wenu wa watu wote kulipa
maji kwa viwango sawa unawapotezea
mapato, wapo wanaoyatumia kwa ajili
kumwagilia migomba kasha watalipa sh
3,000 kwa mwezi, ninyi mnaona hilo ni
sahihi,badilikeni”alisema.
Katika baarifa yake kwa naibu waziri
meneja wa Kiliwater, Prosper Kessy
alisema uzalishaji wanakabiliwa na
uzalishaji mdogo wa maji usiokidhi
mahitaji kwani upo upungufu wa mita
za ujazo 13,000 sawa na lita 13,000,000
kwa siku.
Alisema pia wanakabiliwa nupungufu
wa mita za ujazo 22,000 sawa na litaza
ujazo 22,000,000 wakati wa kiangazi na
hivyo kuongeza tatizo la maji kwa
wateja wake.
“Kiwango kikubwa cha asilimia 78 ya
maji yasiyouzwa kutokana na uchakavu
wa miundombinu,wazi wa maji,wateja
wasio na mita na wale wenye mita lakini
hutumia maji kiholela”alisema.
Hata hivyo alisema kampuni hiyo
inahitaji zaidi y ash milioni 600 kwa
ajili ya kuwafungia mita wateja wake
kama njia moja wapo ya kuongeza
mapato

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments