Monday, July 29, 2013

Wafanyakazi wa Benki ya NBC watembelea kituo cha watoto yatima na kuwakabidhi misaada


Wafanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha operesheni, wakipozi kwa picha na watoto wanaolelewa katika kituo cha Ijango Zaidia Orphanage cha Sinza
walipokwenda kupeleka msaada wa vyakula, sabuni, mafuta ya kupikia na vyandarua ikiwa ni moja ya mikakati ya
NBC kurudisha sehemu ya faida
waipatayo katika jamii. Hafla ilifanyika
kituoni hapo jijini Dar es Salaam juzi.
Wengine ni watumishi wa kituo hicho.

Mkurugenzi wa Uendeshaji na Huduma
wa Benki ya NBC Tanzania, Cornie Loots
(kulia) akikabidhi msaada wa vyakula,
mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua
kwa Mkuu wa kituo cha watoto yatima
cha Ijango Zaidia Orphanage , Bi. Zaidia
Nuru Hasani, vilivyotolewa na NBC
kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.

Mtoto anayelelewa katika kituo cha
watoto yatima cha Ijango Zaidia
Orphanage, Ramia Mahmoud , akipokea
mafuta ya ngozi kwa niaba ya wenzake
vyaliyotolewa msaada na Benki ya NBC
kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo,
Ernest Paulo Mbepera (kulia) kituoni
hapo, Sinza, jijini Dar es Salaam. Benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua.

Mfanyakazi wa Benki ya NBC,
Mwanaisha Nassoro Ayosi (kulia)
akikakabidhi misaada iliyotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.

Mtoto anayelelewa katika kituo cha
watoto yatima cha Ijango Zaidia
Orphanage, Amina Twahilu, akipokea
moja ya vyandarua kwa niaba ya
wenzake vilivyotolewa msaada na Benki
ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki
hiyo, Anyelwisye Enock Mwakatobe
(kulia) kituoni hapo, Sinza, Dar es
Salaam juzi. Benki hiyo ilikabidhi
msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia
na sabuni.
Chanzo michuzi blog

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments