Tuesday, August 20, 2013

Basi la Turu lachomwa moto na wanakijiji kulipizia kuuwawa kwa mwenzao


Abiria wapatao 60 waliokuwa
wanasafiri na basi la Turu linalofanya
safari zake kati ya mkoa wa Singida na
Haydom mkoani Manyara,
walilazimishwa kuteremka toka ndani
ya basi hilo na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 ) wa vijiji vitatu tofauti ambao
baadae walilichoma moto basi hilo.

Taarifa toka eneo la tukio zinasema
wananchi hao wa vijiji vya Singa,
Idabagadu na Nkungi mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria
wote wameshuka, walilichoma moto basi
hilo ambalo limetekea sehemu kubwa.

Sababu ya wananchi hao kuchukua
uamuzi huo ni kutokana na basi hilo
kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita.
Chanzo michuzi blog

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments