Tuesday, August 13, 2013

Eto’o atoa kauli kuhusu Chelsea


Samuel Eto’o huenda akaungana na Mourinho kwa mara nyingine
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya
Cameroon Samuel Eto’o huenda
akaungana na kocha wake wa zamani
Mreno Jose Mourinho baada ya kuweka
wazi utayari wake wa kujiunga na
Chelsea endapo nafasi hiyo itajitokeza.
Eto’o amewekwa kwenye orodha ya
wachezaji wanaotarajia kuuzwa na klabu
ya Anzhi Makhachkhala ya Urusi baada
ya bosi wa klabu hiyo kubadili sera ya
usajili toka kwenye kusajili wachezaji
nyota wenye majina makubwa na
wanaolipwa mishahara minono na
kuamua kujenga timu yenye wachezaji
wa bajeti ya chini.
Kwa muda wa miaka miwili Eto’o
amekuwa mchezaji anayelipwa fedha
nyingi kuliko wote duniani baada ya
kukubali kujiunga na Anzhi ya Urusi
akitokea Inter Milan ambako alicheza
kwa miaka miwili baada ya kuondoka
Barcelona.
Kundi la wachezaji raia wa Urusi
wakiongozwa na nahodha wa timu ya
taifa hilo Igor Denisov walianzisha
mgomo baridi ndani ya kambi ya Anzhi
Makhachkhala dhidi ya wachezaji wageni
wanaolipwa fedha nyingi kama Eto’o hali
ambayo imesababisha mwenyekiti wa
timu hiyo kubadili sera ya usajili na
uendeshaji wa timu hiyo.
Sambamba na Eto’o, staa kama Lassana
Diarra, Lacina Traore, Christopher
Sambana wengineo wanatarajiwa kuuzwa
kwa timu zinazowahitaji.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba
siku kadhaa zilizopita Anzhi ilitangaza
kumfukuza kazi kocha wake Rene
Meulenstein ambaye alikuwa amekaa na
timu hiyo kwa mwezi mmoja pekee
akiwa amekuwa kocha mkuu kwa muda
wa siku kumi na sita baada ya kushika
nafasi hiyo kufuatia kujiuzulu kwa kocha
Guus Hiddink.

Mgawanyo wa mshahara anaopata Eto’o
ndani ya klabu ya Anzhi Makhachkhala.


Eto’o anaongoza kwa kulipwa mshahara
mkubwa kuliko wachezaji wote duniani.

Eto’o mwenyewe ameonekana kuvutiwa
na uwezekano wa kuungana na kocha
wake wa zamani ambaye walifanya kazi
kwa mafanikio ndani ya Inter Milan
ambapo klabu hiyo ilitwaa mataji matano
katika kipindi cha misimu miwili.
Chelsea itamsajili Eto’o endapo
itashindwa kumsajili mshambuliaji wa
Manchester United Wayne Rooney
ambaye Mourinho amemtangaza kuwa
chaguo lake namba moja kwenye usajili
wake.
Story za michezo hapa millardayo.com
unazipata kwa nguvu ya Benki ya NMB.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments