Wednesday, August 14, 2013

Polisi bandia anaswa Dar


Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam leo limefanikiwa kumnasa askari bandia akiwa amevaa sare za jeshi la Polisi la kitengo cha usalama barabarani.

Afande huyo akiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa mchana wa leo akila vichwa maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Suleiman
Kova amesema leo majira ya saa moja na nusu asubuhi wamefanikiwa kumkamata
James Hussein mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa Kimara tangi bovu akiwa amevaa sare hizo huku akiendelea na utapeli wa kujifanya askari wa kitengo cha usalama barabarani.

Aidha Kamanda KOVA ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mara wanapomtilia mashaka askari yeyote na pia kuwaomba wananchi kuwataka
askari kwenda nao kituo cha polisi pindi wanapokamatwa na makosa.

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments