Sunday, August 11, 2013

Wafuasi wa Morsi hawataki kupatana


Chama cha rais aliyetolewa madarakani,
Mohammed Morsi, hakikubali juhudi za
kupatanisha zinazofanywa na mmoja kati ya
viongozi wakubwa wa kidini nchini Misri.
Msemaji wa mashauri ya nchi za nje wa chama
cha Bwana Morsi, cha Freedom and Justice
Party, aliuliza ikiwa imamu mkuu wa al-Azhar
kweli hapendelei upande wowote.
Alisema imamu huyo alipanga njama dhidi ya
rais, na aliunga mkono jeshi kumpindua Morsi.
Mohammed Soudan aliongeza kusema kuwa
haikuelekea chama chake kuombwa
kuzungumza wakati viongozi wake wako jela au
wanakabili mashtaka.
Chama hicho ni tawi la siasa la Muslim
Brotherhood.
Bwana Soudan piya alionya kuwa maandamano
ya wafuasi wa Bwana Morsi yataendelea na
kwamba watu wako tayari kufa.
Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Toa maoni yako/ Leave your comments